VIJANA TAMBARANI!
Picha kwa hisani ya google.
Samaki mkunje angali mbichi na mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.Hizi ndizo fikra ambazo hukita mizizi akilini mwetu sie wakenya pindi tu jina "kijana" linapotamkwa.Kwa miaka na Mikaka Sasa taifa la Kenya kupitia serikali tawala imekuwa ikijitokeza kinaganaga na kudai kubuni nafasi zaidi za ajira kwa kizazi cha baadaye ambao ni vijana zilizosalia kuwa ndoto za mchana kutekelezwa.Imesalia tu kama kumbukizi kwa dhana kuwa "kazi kwa vijana....pesa kwa wazee" ikijidhihirisha waziwazi kama meno ya ngiri.Suala Hilo limegeuka na kuwa donda sugu linalopaswa kuzingatia kikamilifu.
Wasemavyo walumbi,mgala muuwe na haki umpe.Yapasa husika kuingilia kati na kubuni nafasi mbalimbali za ajira kwa kizazi cha baadaye.Hili litawawezesha kupata kipato cha kujimudu kimaisha.Ikilinganishwa kuwa taifa letu lina idadi kubwa ya vijana, itasaidia pakubwa kuboresha na kuimarisha uchumi kwa jumla.Walinena walumbi, Safari ya kesho huandaliwa leo.Kuwapa ajira kutazidisha Pato la taifa litakalochangia taifa kujimudu kiuchumi.
Wakongwe wa jadi hawakutuvisha vilemba vya ukoko walipoamba, nazi mbovu harabu ya nzima.Vijana wana mchango mkubwa zaidi katika ujenzi wa taifa.Iwapo watatimiziwa ahadi mbalimbali Pana uwezekano pakapungua visa vya wizi na utovu wa usalama kwani wengi hujihusisha na uhuni huo kwa kukosa tonge la kutia domoni.Ajira na miradi mbalimbali kwetu sie vijana kutapunguza kama si kumaliza visa vya wizi ambavyo huzorotesha uchumi wa taifa letu.
Siku zote watakwambia, "udongo upatilize uli maji".Nina maana gani kwa kauli hii?Malezi bora na mwongozo dhabiti kwa vijana husaidia kutoa maadili na maarifa kwa kizazi kijacho.Wao ndio viongozi na wazazi wa kesho.Hivyo basi ukwasi wao wa maadili utaipa msukumo na mwelekeo mwafaka nchi hivyo kuinua hadhi kutokana na uongozi Bora na hivyo kuboresha uchumi.
Ngoma ikipigwa Sana mwishowe hupasuka.Naomba serikali kuu kupitia rais William Ruto kulivalia njuga suala la vijana na kutoa suluhu la kudumu.Miradi mbalimbali na nafasi za ajira zibuniwe ili kuwanufaisha wao kwenye nia ya kuimarisha na kuboresha uchumi.Kwani uchumi ni uti wa mgongo wa taifa letu.
Ni mie Shem Felix Ashikumba, mwanafunzi kutoka kitengo cha habari na mawasiliano kwenye chuo kikuu cha ufundi Mombasa (Technical University of Mombasa)TUM.
Kazi safi
ReplyDeleteKazi safi kaka
ReplyDeleteKazi Nzuri Sana
ReplyDeleteSwadakta
ReplyDeleteSafi
ReplyDeleteHongera,Ujumbe mzito na wenye mnato ila punguza kupachika msamiati pahali pasipofaa
ReplyDeleteKazi nzuri sana
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteSafiii kaka
ReplyDeleteNakala Safii
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi nzuri hii daaaaah
ReplyDeleteSwafi
ReplyDeleteSwadakta!!
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteHujawai kosea kaka
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteSadakta. Makala mazuri sana
ReplyDeleteChonjo
ReplyDeletehongera kwa kazi safi
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteWell done Shem Felix
ReplyDeleteWow
ReplyDeleteKazı murua
ReplyDeleteKazi safiii
ReplyDeleteSafiiii
ReplyDeleteNice article
ReplyDeleteWell written
ReplyDeleteNice article
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteThanks guys for your kind support 🙏🙏🙏
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteHeko!kazi safi
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteNakala Safi
ReplyDelete