ELIMU PATAPOTEA!
Picha nikiwa chuo Cha ufundi Mombasa. Kwa kweli,safari ni hatua na kila hatua ni dua.Nina maana gani na kauli hii?Leo hii nimeamua kujitokeza waziwazi na kuiweka paruwanja safari ya masomo yangu ya chuo kikuu.Nikikupakulia na na kuyadadavua kinaganaga usiyoyafahamu kiundani.Asilimia kubwa wakisalia kuwa ni hadithi za Abunwasi na kumbukizi zisizoaminika katu.Waama,kitanda usichokilalia hujui kunguni wake. Masomo ya chuo kikuu ni baadhi ya malengo ya kila adinasi aushini.Nimekuwa mshawasho na ari ya kupata elimu ya vyuo vikuu pindi tu baada ya kukamilisha masomo yangu ya shule ya upili.Nikitaka niyaonje mandhari hayo kwa udi na uvumba kutokana na habari za kutia moyo nilizozipata kutoka kwa watangulizi wangu.Kumbe nilikuwa najipalia makaa. pichani nikiwa kwenye vidato chuo kikuu Cha ufundi Mombasa baada ya kipindi. Maji yalianza kumwagika pindi tu baada ya kusajiliwa chuoni na kukosa vifaa muhimu vikiwemp kipakatalishi na rununu hitajika nikitaja tu baadhi.Iweje n...