HALUA CHUNGU VYUONI.

          Naitwaa tena kalamu tayari kumwaya wino,mara hii nikiwa nimesonya na kusononeka moyoni.Kwani kulikoni?Kwa muda Sasa taifa letu la Kenya limekuwa likiitathmini elimu kama sekta adhimu nchini Hasa Sana kwa ukuaji  na uboreshaji wa uchumi.Namaanisha Nini kwa usemi huu?Elimu ya ngazi ya juu imepewa kipaumbele nchini si tu vyuoni bali hadi kwenye taasisi anuwai za masomo.
          Sie wakenya tumeingiwa na ukasumba na ukiritimba potovu kuwa wana wetu wakifuzu na kuitwa kwenye vyuo vikuu basi pana tumaini la maisha bora ya baadaye pasi na kufahamu ni yepi hutokea pindi tu wanapojiunga na vyuo hivyo kwa tukisahau kuwa ufanisi huhitaji jitihada,bidii na ukakamavu masomoni.
          Kwa sasa elimu ya vyuo vikuu imegeuka na kuwa karaha kwetu sie  wasomi.Mbona hivyo?Sie wanafunzi twajisahau na kujiingiza kwenye lindi la mapenzi na kukosa kutafakari kiini  hasa Cha kujiunga na taasisi hizo.Wengi wetu tunajikita kwenye shughuli za kiutu uzima kama vile mapenzi ya kiholela  ukiachia  mbali kuoana kwa dhana kuwa sir ni watu wazima,tusijue kuwa nazi huharibika ukubwani.
          Mwisho wa kwisha,tunasalia kuwa debe tupu na kuwa Ganda la muwa kutokana na madhara ya  kuambukizwa magonjwa ya zinaa,mimba za kiholela, matokeo duni darasani,kukosa kufuzi kwa kutokamilisha masomo na vifo vya wapenzi kuuana nikitaka tu baadhi.
          Nimekereketwa main na kutiririkwa na mvua ya majonzi kwa maovu tunayotekekeleza sie wasomi kutoka taasisi mbalimbalu hapa nchini.Ni Mola tu atuepushie.Tukumbuke lengo letu maishani na kutafakari magumu wanayopitia wazazi kuhakikisha kuwa karo inapatikana kufanikisha ndoto zetu jambo linalowafanya wakose hata kopo la maji kwa kutujali sie tusiejijali.Mwenyezi mungu turehemu.
             Inatupasa tukumbuke maelfu  na mamilioni ya mapeni wanayolipa wazazi ili kufadhili elimu yetu kwa kutambua kuwa mtaka yote hukosa yote na tujukumikeni kwa kuzingatia yaliyotupeleka chuoni.Natumai washikadau kutoka sekta ya elimu wataufikisha ujumbe huu kwa wanafunzi kutoka  vyuo vyote nchini nikiwa na imani kuwa tutabadilika baada ya kusoma ujumbe huu. Kila la heri.
Ni mie Shem Felix Ashikumba,mwanafunzi kutoka kitengo Cha habari na mawasiliano kwenye chuo kikuu Cha ufundi Mombasa (Technical University of Mombasa)TUM.

Comments

  1. Mhariri wangu ashaeleza aliye na masikio naa afanye nini .....

    ReplyDelete
  2. Something must kill a man kama tunavyosema kwa kimombo, na wakati huu naona ni mapenzi juu wueh!

    ReplyDelete
  3. Ni kweli
    Tufikirie shida wanazo pitia wazazi kwanza

    ReplyDelete
  4. Good work Kirangi blogs 🙏 May God inspire you to keep moving

    ReplyDelete
  5. Kiswahili kitukuzwe.... Mwandishi bora wewe

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TABASAMU TAANUSI KWA WAPWANI!

CHOZI LA DAMU!

VIJANA TAMBARANI!