CHOZI LA DAMU!

Picha angavu kwa hisani ya mamlaka ya kukabiliana na majanga NDMA.
                    Nainamisha kichwa tayari kutema madini, Mara hii nikiwa nimejawa na lindi la mawazo na maswali chungu nzima nisipate hata jawabu.Kulikoni? Wasemavyo walumbi, mbiu ya mgambo ikilia lazima pawe na jambo.Si jambo tu.Ni suala ambalo lafaa litiliwe mkazo na hatua madhubuti kuchukuliwa ili kukabili tatizo hili.Jangwa la ukame limekuwa tishio kubwa nchini huku likikithiri si tu magazetini, kwenye vyombo vya habari na hata semasema za mtaani.
                   Jangwa la ukame limekuwa donda sugu nchini kwa miaka na mikaka Sasa.Hayawani, Mifugo na kadhalika wakiachwa hohehahe bila mbele wala nyuma na hivyo kuishia kupoteza uhai kama si kudhoofika kiafya tu.Ni mwaka huu ambapo majimbo mbalimbali yameripotiwa kuathirika.Kaunti hizo ni pamoja na; Baringo, Isiolo, Marsabit, Garissa, Wajir, Mandera, Tana River, Samburu, Turkana, West pokot, Laikipia, Kitui, Kwale, Embu,Narok,Meru, Tarakanithi, Taita Taveta, Lamu, Makueni, Kilifi na Kajiado.Hii ikijitokeza waziwazi kama meno ya ngiri jinsi wakenya wanateseka na jangwa hili.
                    Waswahili husema, ukiona vyaelea jua vimeundwa.Hivyo basi, ukiona madhara jua pana vyianzo vyake.Ukame umesababishwa na ukosefu wa mvua ya kutosha maeneo mbalimbali nchini na hivyo udongo kukosa rutuba na kuchangia kukauka kwa mimea ambayo ndio tegemeo kuu kwa binadamu na mifugo kama chakula kwa maisha yao ya kila siku huku kukishuhudiwa vifo vya kiholela kwa mifugo na binadamu kutokana na baa la njaa.
                    Mkurupuko wa nzige nchini umechangia kwa kiwango kikubwa zaidi ongezeko la ukame maeneo mbalimbali.Hii ni kutokana na wadudu hao kuvamia mimea ya wakazi bila huruma na kuharibu na kuwafanya kukosa tegemeo halisia la kukithi maisha yao kwa miaka na mikaka.Jambo lililovutia baa la njaa kwa wakazi na mifugo maeneo hayo.
                     Vilevile,kukauka kwa mimea kumeacha ardhi bila Kinga na kuchangia visa vya mmomonyoko wa udongo.Hali hii imepelekea kutokea kwa dhoruba inayobeba kiasi kikubwa Cha mchanga na vumbi kwenye angahewa hivyo kupeleka yenye rutuba penginepo na kuongeza magonjwa ya mfumo wa upumuaji kutokana na vumbi hewani.
picha angavu kwa hisani ya mamlaka ya kukabili majanga nchini.NDMA.
                   Kabla ya kulikunja jamvi,wahenga husema maji ukiyavulia nguo yaoge,shughuli za kibinadamu kama vile ukataji wa miti kiholela na uvamizi wa misitu na binadamu kama makazi umechangia pakubwa sana kushuhudiwa kwa kwa ukame nchini ikichagizwa na mkurupuko wa moto ya misitu na kuacha ardhi ikiwa tambarare.

Athari za ukame ni nyingi zaidi lakini nimekutajia baadhi tu kwa ajili ya muda.Naziomba serikali za kaunti husika kwa ushirikiani na serikali kuu na mamlaka ya kukabiliana na majanga  nchini NDMA kuingilia kati na kutoa suluhu ili kuyaokoa maisha ya binadamu na husika.
Ni mie Shem Felix Ashikumba, mwanafunzi kutoka kitengo Cha habari na mawasiliano kwenye chuo kikuu Cha ufundi Mombasa (Technical University of Mombasa)TUM.
              
                    

Comments

  1. Kaka, serikali kuu na hata mashirika mbali mbali ya kimataifa yameingilia kati kusaidia waathiriwa. Ila sisi kama wananchi inapaswa tuwajibike kuangamiza hili baa la njaa humu nchini.
    Kasi safi

    ReplyDelete
  2. Thanks to all for the support,I won't take it for granted 🙏🙏🙏

    ReplyDelete
  3. Serikali yafaa kujiandaa na mikakati🔥🔥🔥

    ReplyDelete
  4. Kweli ,kukauka kwa mimea kumeacha ardhi bila Kinga na kuchangia visa vya mmomonyoko wa udongo...kazi mufti

    ReplyDelete
  5. Thanks again for your kind support

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TABASAMU TAANUSI KWA WAPWANI!

VIJANA TAMBARANI!