KILIO CHA WANYONGE.
Lisemwalo lipo na kama halipo laja.Mbona hivyo?Kwanza,naanza kwa kukupongeza ewe Rais William Ruto kwa kuibuka mshindi kwenye uchanguzi mkuu wa agosti Tisa.Na Sasa macho yote yameelekezwa kwako baada ya kuaminiwa na kutwikwa jukumu la kuongoza baada ya kuyaweka paruwanja manifesto na ajenda zako kwa wakenya achia mbali ukakamavu,ukomavu,hekima na msimamo wako dhabiti wa kisiasa.Heko kwa Hilo.
Mheshimiwa rais,ilidhihirika wazi tu kama meno ya ngiri kwenye sakasaka zako katika safari ya kuingia ikulu wakati ukimrai na kumuahidi "Wanjiku" kuwa utashughulikia mahitaji yake huku maneno kama"mama mboga" na "bodaboda" yakikita Kambi kinywani kwenye Nia ya"bottom up economy",ukimuahidi mlalahoikuwa kwa kipindi siku mia moja pindi tu baada ya kula kiapo,utatekelezs masuala kama kupunguza bei ya bidhaa muhimu ikiwemo unga,kuwateua majaji zaidi kutaja baaadhi tu.
Kiapo umekila,umefanya ya kufanya yakiwemo kuwateua majaji, kupunguza bei ya pembejeo na mengi ambayo muda umenipa kisogo kuyataja.Hongera bwana rais,si kwamba tu ni kukusifia,bali ni ahadi ilifaa utekeleze kwa wakenya kwani ahadi ni deni.Yote Tisa......kumi,mbona kilio kinazidi? Walalahoi wanazidi kutaabika na kutapatapa ili kutia tongue mdomoni kutokana na gharamu za maisha.Nina imani mtukufu rais,kabla ya kutamatika siku mia moja,utakuwa umelikupia jicho suala Hili na kutoa suluhu ya kudumu kwani yamekamilika majuma mawili tu na siku za kuhesabu tangia ule kiapo.Sie hatuna budi ila kuwa wavumilivu na subira kwani mvumilivu hula mbivu na subira huvuta kheri.
Ni juzi tu kaliteua Baraza lako la mawaziri tayari kwa utendakazi kwani waswahili husema jiya moja haliinjiki chungu na ukitaka kufika mbali.....tembea na wenzio Bali si pekee yako.Wakenya tuna imani kuwa uliowateua watachangia pakubwa kuimarisha na kuboresha uchumi Bali si kuwa tu vikaragozi na mawaziri hewa ndani ya serikali yako.Shukrani kwa kuzingatia usawa wa maeneo na jinsia katika uteuzi wa Baraza lako pasi na kuzingatia Tabaka wala dini licha ya kumsahau Wanjiku kwa Nia ya mama mboga na bodaboda.
Ma'am,Ngoma ikipigwa Sana mwishowe hupasuka,naomba nilikunje jamvi kwa Leo.Tupatanetena baadaye juma lijalo kwa makala Babukubwa nikitumai kuwa washikadau watamfikishia rais ujumbe huu kwa manufaa ya Wanjiku.Muwe na siku njema.
Ni mie Shem Felix Ashikumba,
Mwanafunzi kutoka kitengo Cha habari na mawasiliano.Chuo kikuu Cha ufundi Mombasa.(Technical University of Mombasa)TUM.
Kazi nzuri👍
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteNyc
ReplyDeleteGood work. Keep it up
ReplyDelete🔥🔥
ReplyDeleteKiswahili 🔥🔥
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteThanks to all🙏🙏🙏
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDelete