TABASAMU TAANUSI KWA WAPWANI!
Wasemavyo walumbi nyumbani ni nyumbani tu hata kama ni pangoni na kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.Imesadifika tu kama hekaya za Abunwasi kwetu sie wapwani huku tukisalia tumeduwaa na kubung'aa falauka mzungu wa reli tusiamini kutokana na furaha chekwachekwa iliojaa moyoni.Walilonga waswahili kuwa,lisemwalo lipo na kama halipo laja.Nakusihi uketi kitako ewe msomaji wangu nikudadavulie yaliyomo!
Ni miezi miwili tu tangie sie wapwani na wakenya kwa ujumla kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa agosti tisa huku kilio chetu wapwani kikiwa ni halwa tamu tulionyang'anywa kinywani na kupelekewa wakazi wa Naivasha kwenye nia ya huduma za halmashauri ya bandari nchini (KPA).Ama kweli chozi la samaki haliendi bure majini.
Nakumbuka tu kama jana jinamizi lililotufyonza sie wapwani pindi tu baada ya huduma za halmashauri ya bandari jijini Mombasa kupigwa teke na rais mstaafu Uhuru Kenyatta tukalazimisha kusalia wapweke tusiwe na 'a' wala 'b'.Uchochole ukakita mizizi na kutufanya tukose hata tonge la kutia domoni kutokana na gharamu za maisha zilichangiwa na ukosefu wa ajira.Vijana tulilazimika kujiingiza kwenye gege la ugaidi ikiwemo uporaji na wizi wa kimabavu uliosababisha visa vingi vya utovu wa usalama na uzorotaji wa kiuchumi, nikitaja tu baadhi.
Pongezi ewe amiri mkuu wa jeshi la kitaifa rais William Ruto kwa kutoa amri ya kurejeshwa kwa huduma za halmashauri ya bandari nchini kwa wakazi wa pwani.Heko kwako rais.Ni raha ilioje kwetu sie wapwani? Natumai shughuli za kawaida zitarejelewa huku wapwani tukinufaika kwenye halmashauri hiyo na kuimarisha maisha na uchumi wa ukanda huo huku nafasi za ajira zilizosambaratishwa zikitengwa upya.
Sie wapwani twawaomba washikadau wamfikishie shukrani rais William Ruto tukimsihi azidi kutekeleza ajenda alizoahidi wakenya bali si kwetu wapwani tu ili kufanikisha ustawishaji na uboreshaji wa uchumi wa taifa.Kila la kheri rais.
Ni mie Shem Felix Ashikumba, mwanafunzi kutoka kitengo Cha habari na mawasiliano, kwenye chuo kikuu Cha ufundi Mombasa (Technical University of Mombasa) TUM.
Fantastic
ReplyDeleteSuwadakta
ReplyDeleteKazi nzuri sana kaka
Safiiii mkuu
DeleteKazi safiii
ReplyDeletehongera kwa kazi nzuri
ReplyDeleteGood job
ReplyDeleteTrue dat
ReplyDeleteNice one.
ReplyDeleteNice piece
ReplyDeleteNice work
ReplyDeleteNice article
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteGood
ReplyDeleteTafsiri nzuri na yenye ufasaha. Hongera.
ReplyDeleteAsante sana🙏🙏
DeleteBabaee kiswahili daah
ReplyDeleteLugha mufti
ReplyDeleteNice article
ReplyDeleteKazi safii 👏👏
ReplyDelete👏👏👏
ReplyDeleteKaz murua na safi
ReplyDeleteNakala nzuri
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteGood job
ReplyDeleteKazi salfi mkuu
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteGood
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteThanks for the support
ReplyDeleteGreat article 😊
ReplyDeleteKweli kabisaa
ReplyDeleteGood one
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteUhandishi uko juu
ReplyDeleteHongera, kazi safi kaka
ReplyDeleteNice piece
ReplyDeleteNice article
ReplyDeleteNakala Safi kweli
ReplyDeleteNice article👏
ReplyDeleteNice article 👍
ReplyDeleteNice article
ReplyDeleteKazi safi 👌🏻👏🏻👏🏻
ReplyDeleteThanks all for the support 🙏🙏
ReplyDeleteSafi kabisa
ReplyDeleteSmart article
ReplyDelete🔥🔥💯
ReplyDeleteUandishi mzuri
ReplyDeleteMhenga shem✅
ReplyDeleteGreat
ReplyDeleteHongera 👏Safi sana
ReplyDeleteGood article
ReplyDeleteChonjo wa ingo
ReplyDelete🙌
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteAmazing article 💯💯
ReplyDeleteThanks all once again🙏🙏🙏
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteKazi Safi
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDelete