ELIMU PATAPOTEA!

Picha nikiwa chuo Cha ufundi Mombasa.

Kwa kweli,safari ni hatua na kila hatua ni dua.Nina maana gani na kauli hii?Leo hii nimeamua kujitokeza waziwazi na kuiweka paruwanja safari ya masomo yangu ya chuo kikuu.Nikikupakulia na na kuyadadavua kinaganaga usiyoyafahamu kiundani.Asilimia kubwa wakisalia kuwa ni hadithi za Abunwasi na kumbukizi zisizoaminika katu.Waama,kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.

Masomo ya chuo kikuu ni baadhi ya malengo ya kila adinasi aushini.Nimekuwa mshawasho na ari ya kupata elimu ya vyuo vikuu pindi tu baada ya kukamilisha masomo yangu ya shule ya upili.Nikitaka niyaonje mandhari hayo kwa udi na uvumba kutokana na habari za kutia moyo nilizozipata kutoka kwa watangulizi wangu.Kumbe nilikuwa najipalia makaa.
pichani nikiwa kwenye vidato chuo kikuu Cha ufundi Mombasa baada ya kipindi.

Maji yalianza kumwagika pindi tu baada ya kusajiliwa chuoni na kukosa vifaa muhimu vikiwemp kipakatalishi na rununu hitajika nikitaja tu baadhi.Iweje nisajiliwe bila vifaa hivyo na ilhali ilikuwa baadhi ya vigezo.Ni swali ambalo Hadi Sasa sijawai pata jawabu mwafaka jinsi jinsi nilipenya bila vifaa hivyo kati.Kwa kweli Mungu si athumani.Alhamdhullillahi.

Nukta ilibadilika na kuwa sekunde,sekunde ikawa dakika,dakika zikajihesabu na kuwa siku,siku ikageuzwa na kuwa wiki,wiki ikaliwa na kuwa miezi,miezi ikageuzwa na kuwa miaka.Kadri muda uliyoyo ndivyo ndivyo mwelekeo zaidi wa vitushi ulijengeka kwa Kasi.Maisha chuoni yakaanza kunipiga chenga.Ikageuka kuwa kama ibaada kwangu kuelekea malazini kujipumzisha bila  hata kutia tone la maji domoni kwa kukosa Hela za matumizi ukiachia mbali za kufadhilisha masomo yaliyohitaji maelfu ya mapesa pindi tu kila baada ya kipindi Cha miezi mitatu ndani ya mwaka mmoja.Nikalazimika kuupiga moyo konde liwalo na liwe kwa kutafuta vibarua mradi nipate vipeni viwili vitatu vya kunisitiri na kunisaidia kugharamikia elimu yangu.Kwani haha na haba hujaza kibaba.
pichani baada kutoka vibarua vya kujikimu maishani.

Imekuwa ni safari ya pandashuka nikilazimika kuikwea milima na mabonde.Nikilazimika Mara si haba  kukwepa vipindi chuoni kwa kujishughulisha na kazi za kijungujiko mwisho wa kwisha nikiwa na imani kuwa likupigalo ndilo likufunzalo na mume ni mume japo anastahili sifa za gumegume.

Ni mengi zaidi ningependa kuyasimulia kunihusu lakini kwa ajili ya muda ningependa nitie kitone kwa Leo.Imani na matumaini yangu yakiwa  kutimiza malengo ifikapo wakati mwafaka manapo majaliwa yake Allah.Inshaaalllah.

Ni mie Shem Felix Ashikumba, mwanafunzi kutoka kitengo cha habari na mawasiliano kwenye chuo kikuu cha ufundi Mombasa (TUM).

Comments

  1. Kweli nakubaliana nawe ya kwamba imekuwa ni safari ya pandashuka

    ReplyDelete
  2. Hongera kaka,, Kazi nzuri,, Kweli masomo sio chakula uleteachwo mezani na kumeza tu,,
    Takwimu za kibabu hizo
    swadakta!!!πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ™„

    ReplyDelete
  3. Elimu ndio ufunguoπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

    ReplyDelete
  4. Hongera Kwa kazi Nzuri πŸ‘ŒπŸ‘

    ReplyDelete
  5. La haula kiswahili kitukuzweee daaaaaaah

    ReplyDelete
  6. Thanks all for your support πŸ™πŸ™πŸ™

    ReplyDelete
  7. Simulizi nzuri tena ya kuvutia. Hongera.

    ReplyDelete
  8. Na pia kadri siku sinavyo songa, akili yano inaendelea kujawa na hekima.
    Kazi safi

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TABASAMU TAANUSI KWA WAPWANI!

CHOZI LA DAMU!

VIJANA TAMBARANI!