ELIMU PATAPOTEA!
Picha nikiwa chuo Cha ufundi Mombasa.
Kwa kweli,safari ni hatua na kila hatua ni dua.Nina maana gani na kauli hii?Leo hii nimeamua kujitokeza waziwazi na kuiweka paruwanja safari ya masomo yangu ya chuo kikuu.Nikikupakulia na na kuyadadavua kinaganaga usiyoyafahamu kiundani.Asilimia kubwa wakisalia kuwa ni hadithi za Abunwasi na kumbukizi zisizoaminika katu.Waama,kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
Masomo ya chuo kikuu ni baadhi ya malengo ya kila adinasi aushini.Nimekuwa mshawasho na ari ya kupata elimu ya vyuo vikuu pindi tu baada ya kukamilisha masomo yangu ya shule ya upili.Nikitaka niyaonje mandhari hayo kwa udi na uvumba kutokana na habari za kutia moyo nilizozipata kutoka kwa watangulizi wangu.Kumbe nilikuwa najipalia makaa.
Maji yalianza kumwagika pindi tu baada ya kusajiliwa chuoni na kukosa vifaa muhimu vikiwemp kipakatalishi na rununu hitajika nikitaja tu baadhi.Iweje nisajiliwe bila vifaa hivyo na ilhali ilikuwa baadhi ya vigezo.Ni swali ambalo Hadi Sasa sijawai pata jawabu mwafaka jinsi jinsi nilipenya bila vifaa hivyo kati.Kwa kweli Mungu si athumani.Alhamdhullillahi.
Nukta ilibadilika na kuwa sekunde,sekunde ikawa dakika,dakika zikajihesabu na kuwa siku,siku ikageuzwa na kuwa wiki,wiki ikaliwa na kuwa miezi,miezi ikageuzwa na kuwa miaka.Kadri muda uliyoyo ndivyo ndivyo mwelekeo zaidi wa vitushi ulijengeka kwa Kasi.Maisha chuoni yakaanza kunipiga chenga.Ikageuka kuwa kama ibaada kwangu kuelekea malazini kujipumzisha bila hata kutia tone la maji domoni kwa kukosa Hela za matumizi ukiachia mbali za kufadhilisha masomo yaliyohitaji maelfu ya mapesa pindi tu kila baada ya kipindi Cha miezi mitatu ndani ya mwaka mmoja.Nikalazimika kuupiga moyo konde liwalo na liwe kwa kutafuta vibarua mradi nipate vipeni viwili vitatu vya kunisitiri na kunisaidia kugharamikia elimu yangu.Kwani haha na haba hujaza kibaba.
Imekuwa ni safari ya pandashuka nikilazimika kuikwea milima na mabonde.Nikilazimika Mara si haba kukwepa vipindi chuoni kwa kujishughulisha na kazi za kijungujiko mwisho wa kwisha nikiwa na imani kuwa likupigalo ndilo likufunzalo na mume ni mume japo anastahili sifa za gumegume.
Ni mengi zaidi ningependa kuyasimulia kunihusu lakini kwa ajili ya muda ningependa nitie kitone kwa Leo.Imani na matumaini yangu yakiwa kutimiza malengo ifikapo wakati mwafaka manapo majaliwa yake Allah.Inshaaalllah.
Ni mie Shem Felix Ashikumba, mwanafunzi kutoka kitengo cha habari na mawasiliano kwenye chuo kikuu cha ufundi Mombasa (TUM).
Kazi safi ashikumbaπ
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKweli nakubaliana nawe ya kwamba imekuwa ni safari ya pandashuka
ReplyDeleteHongera kaka,, Kazi nzuri,, Kweli masomo sio chakula uleteachwo mezani na kumeza tu,,
ReplyDeleteTakwimu za kibabu hizo
swadakta!!!π₯π₯π₯π
Kazi nzuri
ReplyDeleteGood piece keep up
ReplyDeleteWell articulated
ReplyDeleteSmart
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteElimu ndio ufunguoπ₯π₯π₯
ReplyDeleteNakala nzuri sana.
ReplyDeleteNakala Safii Ndugu π
ReplyDeleteSwadakta!!
ReplyDeleteHongera Kwa kazi Nzuri ππ
ReplyDeleteKazi njema
ReplyDeleteGood job
DeleteLa haula kiswahili kitukuzweee daaaaaaah
ReplyDeleteHongeraπ
ReplyDeleteWagwanπ
ReplyDeleteKazi nzuri shem
ReplyDeleteThanks all for your support πππ
ReplyDeleteNzuri Sana kaka
ReplyDeleteSimulizi nzuri tena ya kuvutia. Hongera.
ReplyDeleteNa pia kadri siku sinavyo songa, akili yano inaendelea kujawa na hekima.
ReplyDeleteKazi safi
Kazi nzuri
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteWell written. What a journey!
ReplyDeleteKizazi sana
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteInteresting
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteKazi safiii
ReplyDeleteThanks all for your great support
ReplyDeleteNakala Nzuri
ReplyDeleteNakala Safi
ReplyDeletegood job
ReplyDeleteSafii
ReplyDelete